JINSI YA KUTUMA APK WHATSAPP KWA MTU AU GROUP

Habari!

Leo tutajifunza namna ya kutuma APK kwenye group whatsapp au kumtumia mtu binafsi.
Kwa wasioelewa maana ya APK maana yake ni file fulani litakalo muwezesha mtu kuinstall application kwenye simu yake.

Ili uweze kutuma APK kwa njia ya whatsapp yakupasa kwanza kuwa na hiyo APK kwenye simu yako. Si lazima uidownload hiyo APK bali kama una application husika kwenye simu yako unayohitaji kuituma waweza itengenezea APK yake.

Ni kwa jinsi gani nitaitengeneza APK kutoka kwenye APP niliyonayo tayari kwenye simu?

πŸ‘‰Kuna namna nyingi na app nyingi zinazoweza kukusaidia kutengeneza APK kutoka kwenye APP ambayo unayo tayari kwenye simu yako, lakini mimi hapa nitaelekeza kwa kutumia ES File Explorer.

πŸ‘‰ES File Explorer ni APP aminika na pendwa kwa wadau wote wenye maujuzi ya simu hasa ukiwa umeroot simu yako. Hauna haja ya kuwa na APP nyingi kwenye simu yako zenye kufanya kazi ya kujirudia rudia.

Mahitaji:
• Android phone
• Whatsapp app
• ES File Explorer app

Zingatia: Kama hauna moja ya app hapo juu au hazipo updated unaweza kuzipata kwa urahisi kwenye channel yetu ya Android TRICKS Telegram kwa kubinya HAPA. Kama hauna Telegram idownload kwanza kwa kubinya HAPA na ujisajiri.

Fuata hatua zifuatazo kutengeneza APK kutumia ES File Explorer

1. Ifungue APP ya ES File Explorer.

2. Utaona mahali pameandikwa APP binya hapo hapo




3. Zitakuja APP karibia zote zilizopo kwenye simu yako, binya kwa mda kidogo APP unayohitaji kuitengenezea APK mpaka ikuletee alama ya tick. mf. Telegram




4. Kisha binya vidoti vitatu (option) na chagua share




5. Katika machaguo ya kushare chagua "ES Save to..." na subiri utaletewa ukurasa utakao kutaka kuchagua wapi unahitaji kuhifadhi hiyo APK yako.




6. Kwa urahisi zaidi wa kuipata hiyo APK unapohitaji kuituma Whatsapp isave kwenye file la Whatsapp Documents. 
Fungua Internal Storage > Whatsapp/GB Whatsapp > Media > Whatsapp Documents kisha binya "select".
πŸ‘‰ Tazama mfano wa picha mbili hapo chini



7. Mpaka hapo utakuwa umesha isave APK kwenye File la Whatsapp Documents.

πŸ‘‰ Kama utapenda unaweza kwenda kwenye file hilo na kuirename japo sio lazima sana.

KUMBUKA:  Sio lazima uitumie hii njia, kama unanjia nyingine ambayo unaona kwako ni rahisi zaidi kutengeneza APK itumie ila kwa urahisi zaidi wa kuiona hiyo APK Whatsapp ili uitume ihamishe kwenye File la Whatsapp Documents endapo utapata shida kuiona Whatsapp.

JINSI YA KUITUMA APK WHATSAPP

πŸ‘‰ Fuata hatua zifuatazo kuituma APK whatsapp:

1⃣ Fungua Whatsapp/GBWhatsapp yako

2⃣ Nenda mahali unapohitaji kuituma APK iwe kwenye group au kwa mtu binafsi

3⃣ Binya alama ya πŸ“Ž

4⃣ Chagua Documents




5⃣ Itafute APK yako kwenye orodha itakayo tokea na ibofye.



6⃣ Utaulizwa kama unahitaji kutuma file hilo bofya "SEND"



7⃣ Mpaka hapo utakuwa umesha ituma APK Yako




KWA MAUJUZI MENGINE ZAIDI USISITE KUWA UNATUTEMBELEA HAPA HAPA KATIKA BLOG YETU HII KWA KUSEARCH https://superneat2013.blogspot.com

PIA WAWEZA KUUNGANA NASI TELEGRAM KWA KUSEARCH @allabtandroid SEHEMU YA KUSEARCH TELEGRAM

Comments

Popular posts from this blog

MCHONGO WA PESA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA WATER INSTITUTE UBUNGO

HABARI KUHUSU MIKOPO KWA KIDATO CHA SITA WOTE