JINSI YA KUPENDA - 3
Habari!
Ni siku nyingine imempendeza Mungu kupata kibali cha kukuandikieni makala hii ya tatu na ya mwisho katika somo letu la JINSI YA KUPENDA.
Bila shaka umepata kitu katika mfururizo wa somo hili. Usisahau kwamba dhana ya Upendo inazungumzwa kwa namna nyingi sana ila ni juu yako kulinganisha kizungumziwacho na hali halisi iliyopo.
Kama ndio unaungana nasi huwezi pata mtiririko mzuri hivyo ni vyema ukaanza sehemu ya kwanza kwa KUGUSA HAPA
Ebu sasa tujikumbushe tulipoishia wakati uliopita, Tuliona kuna njia tano za kupenda kwa vitendo (hii ni kwa kuanzia, waweza gundua mengi zaidi baada ya kuyafanya haya), na tuliona kipengele cha kwanza cha Kutenda vitendo vya ukarimu, leo hii tutaendelea katika vipengele vinne vilivyosalia na kufunga mada hii. Karibu
2. KUZUNGUMZA KWA MANENO YA UPOLE NA KUSHUKURU
Kila mtu anahitaji kuthaminiwa, Sote hupenda kusikia wenza wetu wakizungumza nasi kwa upole na sio kutukaripia. Lakini pia hujisikia vizuri zaidi pindi wenza wetu wanapo tushukuru kwa yale mazuri tunayo yafanya. Kama mtu atakukaripia hakika utajisikia vibaya na kuumia rohoni.
Mfano: Happy na Zaka walikuwa wakielekea beach pamoja na marafiki zao walipo kuwa hatua chache tu kutoka nyumbai wakiwa kwenye gari alilokuwa anaendesha Zaka, Happy alikumbuka kuwa amesahau mafuta yake ya kujipaka akamuomba mumewe Zaka warudi kuchukua kwakua hawakuwa wamefika mbali... Zaka alijibu hakuna shida tutanunua huko huko mbele. Happy akamwambia "Honey mafuta yangu ni ghari sana sitamani tuingie kwenye gharama hiyo hali ya kuwa ninayo, kwakua hatujafika mbali naomba usimamishe gari mnisubiri hapa mimi niendee sinto chukua muda mrefu kurejea". Zaka alimjibu Happy kwa ukali "Kwanini unakuwa mgumu kuelewa? Kwanini huwezi kuandaa mambo yako vizuri na uanze kusumbua watu". Je! Unafikiri Happy alijisikiaje mbele ya rafiki zake baada ya kujibiwa hivyo na mumewe. Na unafikiri Happy angejisikiaje mbele ya rafiki zake kama Zaka angemjibu kwa upole na kumsifia,,, mf. "Hakika mke wangu Happy upo makini sana hata katika matumizi yetu, ulilosema ni zuri zaidi unaakili sana bebe, ngoja turejee haraka tena hata hatujafika mbali" hakika angejisikia faraja sana mbele ya rafiki zake na angeona anapendwa na kuthaminiwa. Kumbuka mada yetu ni JINSI YA KUPENDA.
Kama utazungumza kwa upole na mwenza wako basi ataona unamthamini na kumpenda. Lawama na malalamiko haviwezi kumbadilisha mwenza wako ila kwa maneno ya upole na kuthamini hilo linawezekana. Chagua leo kuzungumza kwa upole na mwenza wako.
3. KUSAIDIA
Nani asiyependa kusaidiwa pindi anapokuwa anahitaji msaada? Hakika kila mtu hupenda kupewa msaada pindi anapohitaji msaada. Mwenza wako anapohitaji msaada uwe wa kifedha, kimawazo au vyovyote vile usisite kumsaidia kama ni ndani ya uwezo wako. Hii haijarishi kwa mwanaume au mwanamke, mapenzi ni kuhusu kusaidiana pia, sio wakati wa raha tu na chumbani. Upendo wa kweli huonekana wakati wa shida na pindi ambapo watu wote wanakukimbia kwa matatizo uliyoyo lakini akupendae hakukimbii kamwe. Na unaposaidiwa usiache kutoa shukrani kwa mwenza wako. Mwambie asante sana kwa jinsi unavyojitoa kwaajili yangu, nakupenda sana. Mshukuru mwenza wako. Kuwa makini katika kusaidia na kushukuru kwa mwenza wako.
4. KUSAMEHE NA KUACHILIA
Hili nitalizungumzia kwa ufupi kwakua nililizungumza katika sehemu ya kwanza, ila ntakazia tu kwamba ni hatari sana kusamehe peke yake pasipo kuyaachilia yale uliyo yasamehe.
5. KUMKUBALI MWENZIO KAMA ALIVYO
Kila binadamu anamapugufu yake, hakuna binadamu mkamilifu kwa kila kitu, kama utaona udhaifu au kasoro fulani kwa mwenzi wako, usilalamike au kuwa mgomvi badala yake mweleze mwenzio kwa upole na kwa wakati ambao anafuraha jinsi ambavyo ungependa abadilike kwani sio yeye hata wewe pia lazima utakuwa na mapungufu yako ambayo itampasa akuchukulie au kama niyakubadilika atapenda ubadilike. Unapo ongea na mwenza wako juu ya kufanya badiliko fulani katika mwenendo wake pindi tu unapoona badiliko kidogo mpongeze na mshukuru. Na hata kama hautoona badiliko kwani si kila udhaifu hutibika basi endelea tu kumkubali kama alivyo na umpende.
HITIMISHO
Kwa maelezo yote hayo kuanzia sehemu ya kwanza mpaka tunapofikia hitimisho leo hii mimi nasema kupenda wakati mwingine ni chaguo. Si sahihi kwamba huwezi tena kumpenda mwenzi wako wa ndoa au kwamba haiwezekani kurejesha tena upendo uliopotea kwa mweza wako wa ndoa. Japo ni tofauti kidogo kwa wapenzi ambao hawajafunga ndoa kwani mapenzi yao hayana dhamana halisi.
HUU NI MWISHO WA MAKALA HII YA JINSI YA KUPENDA, KWA MAKALA ZAIDI JUU YA MAHUSIANO USISITE KUWA UNATEMBELEA BLOG HII YA superneat2013.blogspot.com
KWA MAONI AU USHAURI AU KWA UHITAJI WA MSAADA WOWOTE TUANDIKIE E-MAIL KUPITIA superneat2013@gmail.com
PIA WAWEZA TOA MAONI YAKO HAPO CHINI
KUSOMA MAKALA YA KWANZA GUSA HAPA
KUSOMA MAKALA YA PILI GUSA HAPA
Comments
Post a Comment