JINSI YA KUPENDA - 1


Utangulizi
Habari, leo ni siku njema ambapo tutazungumzia swala zima la jinsi ya kupenda. Pengine umepata mshangao kidogo baada ya kuona kichwa cha habari na kujiuliza: hivi kuna njia maalumu ya kupenda? Usiwe na mashaka nifuatilie kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa makala hii naamini utanielewa vizuri zaidi na utaboresha upendo kwa mweza wako au pengine kama upendo baina yenu wawili ulikuwa umepotea utashangaa kuona mapenzi baina yenu yamerejea na kuongeza furaha katika mahusiano yenu.

NB: Kwa matokeo mazuri usisome peke yako share na mwenza wako pia kwa kusoma nae kwa sauti mkipokezana kwa zamu huku mkiwa sehemu tulivu zaidi ambapo yaweza kuwa chumbani, beach au sehemu yoyote ilimradi iwe tulivu au pia kama sio hivyo mtumie link asome makala hii ili na yeye atambue nini cha kufanya.

Ili kuelewa jinsi ya kupenda kwanza kabisa lazima utambue maana halisi ya upendo. Je! Umewahi kujiuliza upendo ni nini? Kama jibu ni ndio, ulipata majibu gani kuhusu upendo tafadhali share na mimi kwa kucomment mwishoni mwa makala hii maana ya upendo uliyoipata.

Sasa naomba ufuatane na mimi katika maana halisi ya upendo.

UPENDO
Upendo ni neno moja lakini limebeba vitu vingi ambapo kuacha kuvitekeleza vitu hivyo huondoa maana halisi ya upendo. Upendo ni vitendo, nifuatilie vizuri tafadhali. Upendo ni hali ya kumtendea mtu vitendo vya ukarimu, ni hali ya kuzungumza na mtu kwa maneno ya upole, ni hali ya kutoa, kujali, kusamehe na kuachilia.
Hayo yote yanaleta maana zaidi ya upendo pindi utakapo mfanyia mtu hata kama hujisikii kufanya hivyo. Mfano, Kuongea kwa upole na mwenza wako hata kama amekataa kufanya tendo na wewe kwa wakati huo japo wewe umehitaji. Kwa kawaida hapa mtu atahisi hali fulani ya hasira na hali ya kuzungumza na mwenza wake kwa ukali lakini atakapozungumza naye kwa upole hali ya kuwa msukumo wa ndani unamtaka kuzungumza naye kwa ukali basi huo ni upendo wa dhati. (Isitumike kama kigezo cha kupima upendo kwa mwenzako ni makosa.)

Nielewe hapa tafadhali ninapo sema kusamehe na kuachilia namaanisha ni kumsamehe mtu kwa kile alichokukosea lakini sio kuishia tu kumsamehe na kuvitunza moyoni bali kuvipuuzia. Watu wengi wamekuwa wakiwasamehe wenza wao lakini huvitunza moyoni vile vitu walivyo kosewa hivyo kusababisha hasira zaidi yenye kupelekea maamuzi mabaya zaidi pindi anapokosewa kwa mara nyingine, hii ni kwasababu muhusika huanza kurejesha mawazoni mwake yale makosa yote aliyofanyiwa hapo awali na hii ni mbaya sana wenzetu wanasema too bad na ni miongoni mwa vyanzo vya wapenzi kuachana.

Kumbe basi kama umenifuatilia vizuri upendo ni vitendo lakini sasa upendo mara nyingi huwa unabebwa na hisia. Hisia inayoubeba upendo inaitwa Hisia ya penzi.

HISIA YA PENZI
Hisia ya penzi ni hali ya furaha isiyoelezeka anayokuwa nayo mtu ikiambatana na msisimko moyoni na kujihisi mchangamfu na mwenye furaha sana pindi anapomuona mtu ampendae.
Unaweza kupigiwa simu tu na umpendae ikawa like oh! wao my bby calling, yaani ukawa na furaha tu hata hujui imetoka wapi hii tunaita hisia ya penzi.
Hisia hii asikwambie mtu ni hisia nzuri kuliko hisia zote duniani hasa unapokutana na mtu anayekupenda pia kwa dhati kama umpendavyo.

Zingatia, Hisia ya penzi ni hisia kama hisia nyinginezo. Mfano wa hisia nyinginezo ni hisia ya hasira, huzuni na furaha. Kawaida ya hisia huja na kutoweka, Je! Umewahi kuwa na hasira kwa mwaka mzima? Bila shaka jibu ni hapana kumbe basi hata katika hisia ya penzi ni vivyo hivyo kuna kipindi huja na kunakipindi hutoweka. Mfano bila shaka kuna wakati mpenzi wako akikupigia simu au ukimuona inakuwa kawaida tu lakini kuna wakati unajisikia raha sana na kujiona mchangamfu. Hisia ya penzi inapotoweka usiwe na wasiwasi unachotakiwa ni kuendelea kumpenda mwenzi wako, hisia ya penzi huwa inarejea pasipo kuchukua mda mrefu ilimradi upendo kati yenu uwepo.

UHUSIANO ULIOPO KATI YA UPENDO NA HISIA YA PENZI
Zingatia mfano huu: "Imma na Faraja hawakuwa wanafahamiana kabisa walikutana tu katika kituo cha daladala lakini baada ya kubadilishana namba za simu kadri maisha yalivyozidi kwenda Faraja alionyesha kumjali sana Imma, akawa mkarimu sana, akizungumza na Imma anazungumza kwa maneno ya upole, pale Imma alipomkosea Faraja alisamehewa na kueleweka pasipo migogoro mirefu na hatimae mpaka Imma mwenyewe akaona anapendwa na ikafikia stage kila Imma alipoona simu ya Faraja akajihisi mchangamfu na mwenye furaha sana ikafikia stage akatamani Faraja awe mtu wake.

Kwa mfano huo nahisi utanielewa vizuri zaidi:
Unahisi Imma alijuaje anapendwa? Hapa vitu vilivyomfanya Imma ajue anapendwa ni vitendo vya ukarimu, lugha za upole, msamaha aliokuwa anaupata na kueleweka kwa haraka vyote hivi alikuwa akifanyiwa na Faraja. Vipi kama Imma angekuwa anakaripiwa, na kubezwa, Je! Unahisi angehisi anapendwa na Faraja na Je! Unahisi ingefikia stage akawa anajihisi mwenye furaha na mchangamfu pindi aonapo simu ya Faraja inaita? Bila shaka majibu ni hapana.Kumbe upendo ni vitendo baada ya vitendo hisia ya penzi inaweza kuibuka kwa mtu anayetendewa vitu hivyo kwa mfano Imma alipata hisia ya penzi baada ya kuonyeshwa upendo na Faraja.

KUSOMA SEHEMU INAYOFUATA GUSA HAPA

ONYO: MAKALA HII IMESAJILIWA KUTOLEWA NA KITABU CHANGU KITAKACHO TOKA HIVI KARIBUN, HIVYO BASI KUCOPY NA KUIPASTE BAADA YA TAREHE YA LEO NI KOSA LA JINAI HATUA ZITACHUKULIWA PINDI UTAKAPO BAINIKA. ILA KUSHARE LINK NI RUHUSA.

KWA MAONI, MASWALI, USHAURI COMMENT HAPO CHINI. KAMA UNAHITAJI MSAADA BINAFSI NIANDIKIE E-MAIL superneat2013@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

MCHONGO WA PESA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA WATER INSTITUTE UBUNGO

HABARI KUHUSU MIKOPO KWA KIDATO CHA SITA WOTE