JINSI YA KUPENDA - 2


JINSI YA KUPENDA
           Hebu sasa baada ya utangulizi katika sehemu ya kwanza tulipopata nafasi ya kuangalia maana ya upendo na hisia ya penzi, hivi sasa tuzungumze kwa kina ni kwa njia gani tunaweza kuwapenda wenzi wetu.

Kama huku soma makala ya sehemu ya kwanza GUSA HAPA

Njia halisi za kupenda kwa vitendo ni:
1. Kutenda vitendo vya ukarimu
2. Kuzungumza kwa maneno ya upole na
    kushukuru
3. Kusaidia
4. Kusamehe na kuachilia
5. Kumkubali mwenzio kama alivyo.

1. KUTENDA VITENDO VYA UKARIMU
          Kutenda vitendo vya ukarimu ni njia moja wapo ya kupenda. Siku zote mwanzo wa mahusiano kila mtu huwa mwangalifu sana kutenda vitendo vizuri kwa mwenza wake asije mkosea na ndio maana mwanzoni mwa mahusiano yoyote penzi huwa tamu zaidi lakini baada ya muda mrefu wa mahusiano hayo hali hubadilika. Je! unafikiri unapaswa kuacha kufanya vitendo vya ukarimu baada ya muda fulani? hapana hupaswi kuacha kutenda vitendo vya ukarimu siku zote.

Soma mapendekezo ya nini cha kufanya katika kipengele hiki cha kufanya vitendo vya ukarimu:

WANAUME
  • Mwambie mke wako UNAMPENDA, fanya hivi mara nyingi kadri uwezavyo, na unapomwambia yatazame macho yake mazuri na usionyeshe sura ya ukakamavu toa tabasamu zuri.
  • Msifie mke wako, kuwa maalumu katika sifa zako unazozitoa kwa mke wako, usimsifie kwa kumfananisha na mwanamke mwingine mfanye ajione wa pekee kwako na hauna chaguo lingine zaidi yake.
  • Nendeni matembezini pamoja. Fanya hivi mara kadhaa kwa mwezi au kama unamajukumu mengi sana angalau hata mara moja kwa mwezi. Kwa kufanya hivi mke wako atajihisi bado anapendwa na wewe kiasi kwamba unaweza kutenga muda wa kustarehe pamoja nae.
  • Mletee zawadi mkeo kila iwezekanapo, Imejengeka tabia kwa wanaume kutowapatia zawadi wake zao kwa kujali kwamba huenda zawaidi hii ni ndogo sana. Mwanaume anaradhimika kila mara anapohitaji kumpatia zawadi mke wake kujipanga sana kiasi kwamba anashindwa kutekeleza hilo kwa maana kila anapohitaji kufanya hivyo anajikuta anaahirisha, kumbe basi wapaswa kujua kwamba zawadi ndogo tu inaweza kujenga kitu kikubwa sana kwa mke wako, kwanza kwa kumfanya aone unamthamini lakini mbali na hilo atajua hata ukiwa mbali na yeye unamuwaza kiasi cha kukumbuka kumletea zawadi. Kwa wale ambao wapo katika mapenzi ya mwanamke anakipato kikubwa kukushinda bado sio kitu wapaswa kufanya hivi pia.
  • Tenga muda wa kuzungumza na mkeo, Kama unapata muda wa kuzungumza na marafiki zako katika maswala ya mpira, kubet na mengineyo je! Kwa mke si zaidi. Mawasiliano ni nguzo muhimu sana katika mahusiano, kuwa na muda wa kuzungumza na mkeo, mweleze mawazo na hisia zako naye akueleze pia.
  • Unapokuwa na hasira kuwa mwangalifu kuzungumza naye, Nadhani kila mtu anajua kwamba wakati wa hasira mtu unaweza kuzungunza hata yale ambayo hauku yakusudia, usiwe mtu wa maneno sana hasa unapokuwa na hasira, jaribu kutengeneza mazingira ya kuwaza kwanza kile unachohitaji kukisema wakati wa hasira kwamba kama ungekuwa ndio unaambiwa wewe kingekuwa na madhara gani hasa katika upande wa hisia.


WANAWAKE
  • Mwambie pia mumeo mara kwa mara kuwa unampenda, si kwamba mwanaume pekee ndio anasitahili kukwambia anakupenda. Upendo haupo sehemu moja na kila mtu anahitaji kupendwa hivyo ni furaha ilioje mumeo kusika maneno nakupenda sana tena kutoka kwa yule ampendae.
  • Vaa nguo azipendazo mumeo, Pengine linaonekana kama dogo tu ila linamatokeo makubwa. Unapovaa nguo azipendazo mmeo kutamfanya awe huru na wewe, atajisikia huru hata kutoka na wewe na kuwa na furaha, hii itamfanya awe mwenye tabasamu na kukuona unavutia kila akutazamapo.
  • Wakati mwigine asubuhi mumeo akiwa amelala amka na muandalie chai umletee kitandani ukiwa umeandaa kwenye sinia moja au vyombo vyako maalumu vitakavyo pendezea kumpelekea chai kitandani kisha mwamshe kwa busu zuri huku ukiwa umevaa nguo za kulalia zikiuonyesha mwili wako. Hakika siku njema huonekana asubuhi, utaifanya siku yake iwe nzuri sana na asilimia kubwa ya siku hiyo atakuwa anakuza tu wewe.
  • Usitake kushindana na mume wako, Siku zote usitake kushindana na mume wako, muheshimu kwani huyo ni mumeo hata kama unapesa, madaraka au elimu kumshinda. Kuwa mwangalifu kuzungumza naye hasa mnapozungumza maswala mbayo wewe umemshinda. Kwa mfano mnazungumzia swala lihusianalo na elimu kwa watoto wenu yeye akawa anapinga kitu fulani na wakati huo wewe unamshinda elimu kuwa mwangalifu kuzungumza nae kwani ukizungumza naye kwa kumpinga ataona unajiinua kwake kwakua unamshinda elimu.
  • Mumeo anaporudi nyumbani kutoka kazini mpokee kwa hali ya furaha na uchangamfu huku ukiwa na tabadamu zuri ukimwambia pole na kazi mume wangu bila shaka umechoka nadhani wahitaji kupumzika kidogo kabla ya kufanya chochote... sio mume anafika tu mara unaanza na nilikuwa nakuwaza kweli enhe vipi umekumbuka kupitia mboga za usiku kwa maana pesa haikutosha nilienda na saloon kama ulimpa taarifa hiyo vile.


WOTE
  • Ziachie wazi hisia zako hata kwa watu wa karibu yake, Hapa namaanisha marafiki zake, ndugu zake na hata wazazi wake. Hebu waeleze ni kwa jinsi gani unampenda na kumthamini mwenza wako, Hii itasaidia kumfanya ajue yeye ni wapekee, pia hata inapotokea mgogoro kati yenu kama unavyojua binadamu hatujakamilika itakuwa rahisi kusuluhishwa na watu hao, kwani watakuwa wanaujua ukweli juu ya upendo wako kwake na watakuwa na sababu ya kumshawishi akusamehe.
  • Waeleze wanao kuwa unampenda sana baba/mama yao, kwa kufanya hivi watoto watakuheshimu na kumuheshimu pia baba/mama yao lakini pia watakuwa katika malezi ya kuujua upendo wa kweli kwa vitendo na si kusikia tu.
  • Kama utasikia watu, ndugu, wazazi au marafiki zako wanasema kitu fulani kizuri kuhusu mwenza wako mwambie, usione wivu au kutomwambia ukihisi atajivuna bali utamfanya kujua kile akifanyacho ni kizuri na itamfanya kuzidi kukifanya kwa ubora zaidi. Kwa mfano kama mwenza wako huwa anaenda kuwa tembelea wazazi wako mara kwa mara akiwa na vijizawadi fulani fulani kisha siku moja mama yako akakwambia mwenzio huwa anakuja mara kwa mara kutuona anamoyo wa upendo kweli na huwa haachi kubeba zawadi.... Usisite kumwambia mwenza wako mama anafurahishwa sana na tabia yako ya kwenda kuwaona mara kwa mara na huwa anapendezwa pia na zawadi unazopeleka.
  • Anafonya kitu fulani kizuri msifie, Jenga tabia ya kusema asante kwa mwenza wako kila anapotenda kitu fulani kizuri. Mwambie asante sana huku ukiyatazama macho yake na ukitoa tabasamu zuri na lenye kuvutia.


KUSOMA SEHEMU YA KWANZA GUSA HAPA

KUSOMA SEHEMU INAYOFUATIA GUSA HAPA

KWA MAONI AU USHAURI AU KWA UHITAJI WA MSAADA WOWOTE KUHUSU MAHUSIANO TUANDIKIE E-MAIL KUPITIA superneat2013@gmail.com

PIA WAWEZA TOA MAONI YAKO HAPO CHINI

Comments

Popular posts from this blog

MCHONGO WA PESA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA WATER INSTITUTE UBUNGO

HABARI KUHUSU MIKOPO KWA KIDATO CHA SITA WOTE