JINSI YA KUTUMA APK WHATSAPP KWA MTU AU GROUP

Habari! Leo tutajifunza namna ya kutuma APK kwenye group whatsapp au kumtumia mtu binafsi. Kwa wasioelewa maana ya APK maana yake ni file fulani litakalo muwezesha mtu kuinstall application kwenye simu yake. Ili uweze kutuma APK kwa njia ya whatsapp yakupasa kwanza kuwa na hiyo APK kwenye simu yako. Si lazima uidownload hiyo APK bali kama una application husika kwenye simu yako unayohitaji kuituma waweza itengenezea APK yake. Ni kwa jinsi gani nitaitengeneza APK kutoka kwenye APP niliyonayo tayari kwenye simu? 👉Kuna namna nyingi na app nyingi zinazoweza kukusaidia kutengeneza APK kutoka kwenye APP ambayo unayo tayari kwenye simu yako, lakini mimi hapa nitaelekeza kwa kutumia ES File Explorer. 👉ES File Explorer ni APP aminika na pendwa kwa wadau wote wenye maujuzi ya simu hasa ukiwa umeroot simu yako. Hauna haja ya kuwa na APP nyingi kwenye simu yako zenye kufanya kazi ya kujirudia rudia. Mahitaji: • Android phone • Whatsapp app • ES File Explorer app Zingatia: ...