BODI YA MKOPO YAONGEZA SIKU 7. MAOMBI YA MKOPO MPAKA SEPT. 11

Bodi ya Mkopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), Leo yatangaza kuongeza muda wa kuomba mkopo kutoka 04/09/2017 kama ilivyotangazwa awali mpaka 11/09/2017 ikiwa ni nyongeza ya siku 7.

 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya mikopo mwenge jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya mikopo Bw. Abdul-razaq Badru alidokeza pia idadi ya maombi yaliyokuwa yamepokelewa na bodi mpaka kufikia tarehe 29 mwezi wa nane kwamba yalikuwa maombi 50,000.

Waombaji wote wa mikopo mnashauriwa kuzidisha umakini katika kuomba mikopo yenu ili kuepuka makosa yasiyo ya lazima.

Kama unahitaji kuendelea kuwa karibu na stori mbalimbali katika maisha ya kila siku usisahau ku subscribe katika blog yangu kwa kuweka e-mail sehemu ya juu iliyoandikwa subscribe. Pia tunathamini sana maoni yako. #Bakinasisi

Comments

Popular posts from this blog

MCHONGO WA PESA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA WATER INSTITUTE UBUNGO

HABARI KUHUSU MIKOPO KWA KIDATO CHA SITA WOTE