Posts

Showing posts from August, 2017

BODI YA MKOPO YAONGEZA SIKU 7. MAOMBI YA MKOPO MPAKA SEPT. 11

Image
Bodi ya Mkopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), Leo yatangaza kuongeza muda wa kuomba mkopo kutoka 04/09/2017 kama ilivyotangazwa awali mpaka 11/09/2017 ikiwa ni nyongeza ya siku 7.   Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya mikopo mwenge jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya mikopo Bw. Abdul-razaq Badru alidokeza pia idadi ya maombi yaliyokuwa yamepokelewa na bodi mpaka kufikia tarehe 29 mwezi wa nane kwamba yalikuwa maombi 50,000. Waombaji wote wa mikopo mnashauriwa kuzidisha umakini katika kuomba mikopo yenu ili kuepuka makosa yasiyo ya lazima. Kama unahitaji kuendelea kuwa karibu na stori mbalimbali katika maisha ya kila siku usisahau ku subscribe katika blog yangu kwa kuweka e-mail sehemu ya juu iliyoandikwa subscribe. Pia tunathamini sana maoni yako. #Bakinasisi

HATIMAE MIKOPO KUANZA KUOMBWA KESHO TAR.06/08

Image
          Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetangaza mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 na itaanza kupokea maombi ya mikopo kuanzia 06/08/2017 hadi 04/09/2017.           Waombaji wote wa mikopo watarajiwa mnasisitizwa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 pamoja na taratibu nyingine za uombaji mkopo kabla ya kujaza fomu za maombi ya mkopo zinazopatikana kwenye mtandao wa  https://olas.heslb.go.tz           Kusoma mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 bofya  hapa           Kusoma hatua za kufuata kufanya maombi ya mkopo na malipo bofya  hapa           Kusoma kuhusu sifa za msingi za mwombaji kwa:- Kiswahili bofya   hapa Kiingereza bofya   hapa